NAFASI ZA KAZI WILAYANI GEITA- TUMA MAOMBI YAKO MAPEMA - SEPT 2017

NAFASI ZA KAZI WILAYANI - TUMA MAOMBI YAKO MAPEMA - SEPT 2017


NAFASI Z KAZI WILAYA YA GEITA

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita anawatangazia wanachi wote wenye sifa na nia ya kazi katika Halmashauri hiyo ya Geita  kama ifuatavyo

 MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III. (VILLAGE EXECUTIVE III) NAFASI 3.

Sifa za kuingilia moja kwa moja:
- Kuajiriwa wenye elimu ya kidato cha nne (IV)au sita (VI) aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/ Cheti katika moja ya fani zifuatazo:
Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikaliza Mitaa Hombolo, Dodoma au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

Kazi/Majukumu ya kufanya:

a)    Afisa Masuhuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji .
b)    Kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao, Kuwa Mlinzi wa Amani na Msimamizi wa Utawala Bora katika kijiji
c)    Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya Kijiji.
d)    Katibu wa Mikutano na Kamatl zote za Halmashauri ya Kijiji
e)    Kutafsiri"na kusimamia Sera. Sheria na Taratibu
f)    Kuandaa Taarifa za Utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji mali
g)    Kiongozi wa wakuu wa Vitengo vya Kitaalam katika Kijiji.
h)    Kusimamia. kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za Kijiji.
i)    Mwenyekiti wa Kikao cha Wataalamu waliopo katika Kijiji
j)    Kupokea, kusikiliza na kutatua'jualalamiko na migogoro ya Wananchi
k)    kusimarnia utungaji wa sheria ndogoza kijiji.
l)    Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.

2. MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA III  - NGAZI YA MSHAHARA NI TGS B NAFASI 1

SIFA ZA MWOMBAJI

- awe na elimu ya kidato cha 4
- awe na cheti cha utunzaji kumbukumbu kati ya mojawapo ya fani za Afya, Masijala na mahakama ya Ardhi kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali
- awe na umri usiozidi miaka 45

MAJUKUMU
- kutafuta kumbukumbu/nyaraka/mafaili yanayohitajiwa na wasomaji
- kuthibiti upokeaji, uandikishaji wa kumbukumbu /nyaraka
- kuchambu/kuorodhesha na kupanga  kumbukubmu/ nyaraka katika makundi kulingana na somo hisika kwaajili ya matumizi ya ofisi
- kuweka/kupanga kumbukumbu/nyaraka katika reki (file racks/ cabinets) katika masijala  na sehemu za kuhifadhia kumbukumbu
- kuweka kumbukumbu (barua, nyaraka nk) katika mafaili
- kushughukilia maombi ya kumbukumbu/nyaraka za taasisi au serikali

MAMBO YA KUZINGATIA
- barua ziandikwe kwa mkono
- barua za maombi ziambatanishwe na nakala za vyeti vya elimu, taaluma, cheti cha kuzaliwa na picha mbili za rangi za hivi karibuni
- barua za maombi zaimbatanishwe na maelezo binafsi
- kwa waombaji waliosoma nje ya nchi wahakikishe vyeti vyao  vimehakikiwa na NECTA NA TCU
- Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 20/09/2017 saa 9:30 alasiri

barua za maombi zitumwe kwa anuani ifuatayo

MKURUGENZI MTENDAJI,
HALMSHAURI YA WILAYA YA GETIA,
S.L.P 139,
GEITA

Tangazo hili pia lapatikana kkwenye www.geitadc.go.tz

No comments

ProsperComputerTraining@2016 All right reserved. Powered by Blogger.